Nuclear Abolition News and Analysis

Reporting the underreported threat of nuclear weapens and efforts by those striving for a nuclear free world.
A project of The Non-Profit International Press Syndicate Group with IDN as flagship agency in partnership with Soka Gakkai International in consultative
status with ECOSOC.

logo_idn_top
logo_sgi_top

Watch out for our new project website https://www.nuclear-abolition.com/

About us

TOWARD A NUCLEAR FREE WORLD was first launched in 2009 with a view to raising and strengthening public awareness of the urgent need for non-proliferation and ushering in a world free of nuclear weapons. Read more

IDN Global News

Japan Inasukuma Mafanikio ya Marejeo ya Silaya za Nyuklia ya Marekani

Nuclear Abolition News | IPS
Na Jamshed Baruah*


BERLIN (IPS) – Wabunge na wanaharakati nchini Japan wameonyesha matumaini makubwa kuhusiana na mjadala mkali na unaotegemewa wa U.S. Nuclear Posture Review (NPR) ambao serikali ya Barack Obama imeripotiwa kuwa katika hatua zake za mwisho kuukamilisha.

Chini ya udhamini wa Chama cha Kongres cha Marekani, marejeo haya yataweka mwelekeo wa sera ya Marekani inayohusu silaha za kivita kwa kipindi cha miaka mitano hadi kumi ijayo.

Mapitio ya sera hiyo ya silaha kali yanayoendelea ni ya kwanza kwa takriban miongo miwili baada ya Vita Baridi kumalizika. Serikali za rais Bill Clinton na George W. Bush zilimaliza marejeo ya sera hizo katika miaka ya 1994 na 2001, kila mmoja kwa upande wake.

Japan ni nchi ya kwanza iliyoathirika na mabomu ya nyuklia, katika Hiroshima na Nagasaki mwaka 1945. Ni dhahiri kwamba iko makini kuona nini kinachojiri katika maelekezo ya mazingira na ujumbe wa Marekani – hususan dhidi ya chanzo cha mfululizo wa matetemeko ya mabomu ya atomiki kutoka Korea Kaskazini..

Katika mahojiano ya barua pepe kutoka mji wa Tokyo, nchini Japan, naibu waziri wa zamani wa mambo ya nje nchini Japan Masayoshi Hamada analiambia shirika la habari la IPS: “Uwezekano wa Japan kuhusishwa katika kutokomeza silaha kali ulimwenguni bila kupingwa kuko mbele yetu.”

Hamada, ambaye anawakilisha chama cha upinzani cha New Komei katika Baraza la Madiwani ni miongoni mwa wajumbe 204 wa mabaraza mawili ya bunge la Japan (Diet), aliyeidhinisha barua kwa Rais Obama, Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton, Waziri wa Ulinzi Robert Gates na viongozi wa ngazi za juu wa chama cha Kongres. Barua inaunga mkono kuanzishwa kwa Mazungumzo ya Mkakati wa Kupunguza Silaha (START) kati ya Marekani na Urusi kupunguza idadi ya silaha kali.

Barua yake inafuatilia ya Waziri wa Mambo ya Nje Katsuya Okada kwa Clinton mwezi Desemba 2009. Katika barua hiyo, Okada alijitoa mwenyewe katika serikali ya awamu iliyopita ya Japan ya kusaidia kwa nguvu zote hali halisi ya masuala ya nyuklia ya Marekani, na kuonyesha wazi hisia zake kwamba baadhi ya viongozi wa Japan waliishawishi Marekani kuacha kupunguza silaha zao kali.

“Idadi ya wajumbe 204 haimaanishi kwamba waliobakia wanapingwa na barua au hawakuwa tayari kutia saini,” anasema Akira Kawasaki, mjumbe wa kamati ya utendaji wa Peace Boat, kikundi cha kimataifa kilichopo Japan, na mshauri wa nchi ya Australia na Japan zinazosimamia Kamisheni ya Kimataifa ya Kuzuia Ueneaji na Upunguzaji wa Silaha za Nyuklia. “Ikiwa waanzilishi wa jitihada hiyo wangekuwa na msukumo zaidi, wajumbe wote wa Diet wangeweza kutia saini barua hiyo.

Hans M. Kristensen, mkurugenzi wa Mradi wa Habari wa Silaha Kali katika Shirikisho wa Wanasayansi wa Marekani analiambia shirika la habari la IPS katika mahojiano kupitia barua pepe kutoka Washington: “Barua (ya wajumbe wa Diet) pamoja na matamko ya serikali ya Japan zinatoa mchango mkubwa muhimu wa kupeleka ujumbe wa wazi kwamba mdau mkubwa wa Marekani kutoka Pasifiki hapingi ndoto za serikali ya Obama ya kupunguza silaha za nyuklia lakini anaunga mkono sio tu upunguzaji wa silaha kali bali pia upunguzaji wa ujumbe uliomo katika silaha hizo.”

NPR itahakikisha ahadi ya Marekani ya kuendeleza vizuizi vya silaha kali katika Pasifiki (na mahali pengine) lakini pia Japan inaunga mkono wa kupunguza idadi na ujumbe, Kristemsen amesema katika mahojiano ya barua pepe.

*Makala hii ni sehemu ya mradi wa IPS-Soka Gakkai International wa kutokomeza silaha za nyuklia. Mwandishi ni mwakilishi wa huduma za IDN-InDepthNews anaehusika na masuala ya upunguzaji wa silaha za nyuklia na Japan. (END/2010)

Search

Newsletter

Report & Newsletter

Toward a World Without Nuclear Weapons 2022

Scroll to Top